1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 107 wakiwemo wanawake na watoto wameokolewa Libya

7 Mei 2024

Takriban wahamiaji 107 wakiwemo wanawake na watoto wameokolewa kutoka utumwani katika mji wa kusini mashariki mwa Libya wa Kufra.

https://p.dw.com/p/4fZtV
Boti ya wahamiaji katika bahari ya Mediterania
Shirika la Madaktari wasio na Mipaka limekuwa mstari wa mbele katika operesheni za uokozi katika Bahari ya MediteraniaPicha: Simone Boccaccio/SOPA/IMAGO

Hayo yameelezwa na Walid Alorafi ambaye ni msemaji wa Idara ya Upelelezi wa Jinai huko Benghazi, aliyesema kuwa baadhi ya watu walikutwa na majereha yanayoashiria mateso.

Soma pia: Libya yawarudisha wahamiaji wa Misri nchini mwao

Kulingana na ushuhuda wa baadhi ya wahamiaji, watu hao waliwekwa utumwani kwa karibu miezi saba wakati walipokuwa wakitafuta fursa za kusafiri ili kuingia barani Ulaya. Alorafi amesema wahamiaji hao ni kutoka mataifa ya Afrika yaliyopo kusini mwa jangwa la Sahara wengi wao ikiwa ni kutoka Somalia.

Jiji la Kufra linapatikana karibu kilomita 1,712 kutoka mji mkuu Tripoli. Libya imekuwa ikitumiwa kama njia na wahamiaji wengi wanaokimbia migogoro na umasikini wakitaka kuingia Ulaya, lakini wamekuwa wakikabiliwa na hatari kubwa ya kuvuka jangwa na baadaye bahari ya Mediterania.