1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMexico

RSF yaomba kiongozi ajaye wa Mexico kuwalinda waandishi

Lilian Mtono
27 Aprili 2024

Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka wamemuomba kiongozi ajaye wa Mexico kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na kusambaa kwa mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari.

https://p.dw.com/p/4fF9d
Waandamanaji wapinga mauaji ya waandishi wa habari nchini Mexico
Picha za waandishi wa habari waliouawa nchini Mexico iliyopigwa 2022 huko Mexico City.Picha: Luis Barron/Eyepix/ipa/picture alliance

Kundi hilo la haki za waandishi wa habari, limesema Rais anayemaliza muda wake Andres Manuel Lopez Obrador ameshindwa kuyamaliza mashambulizi hayo.

Kundi hilo limewaomba wagombea watatu kwenye uchaguzi wa urais utakaofanyika Juni 2 kuhakikisha hatimaye wanakuwa na mkakati thabiti wa kuwalinda waandishi wa habari.

Soma pia: Burkina Faso yasitisha shughuli za vyombo viwili vya habari:

Karibu waandishi wa habari 37 wameuawa nchini Mexico tangu Lopez Obrador alipoingia madarakani mwaka 2018.

Kundi hili limeongeza kuwa tangu mwaka 1995, karibu waandishi wa habari 156 wameuawa kwa kufanya habari za uchunguzi wa biashara ya dawa za kulevya na uhalifu mwingine.