1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden asema yuko tayari kupambana na Trump kwenye mdahalo

Lilian Mtono
27 Aprili 2024

Rais Joe Biden wa Marekani amesema yuko tayari kupambana na mgombea mtarajiwa wa urais kupitia chama cha Republican Donald Trump kwenye mdahalo, na kuashiria uhakika juu ya suala hilo.

https://p.dw.com/p/4fF9e
Picha ya pamoja ya Joe Biden na Donald Trump
Picha ya pamoja na Rais Joe Biden na Donald Trump anayetarajiwa kugombea urais kupitia chama cha RepublicanPicha: ABACA/IMAGO;AP Photo/picture alliance

Rais Biden ametoa matamshi hayo alipoulizwa na mtangazaji wa kituo cha Radio cha XM, Howard Stern ikiwa yuko tayari kushiriki mdahalo huo na Trump.

Hadi sasa, timu ya kampeni ya Biden bado haijazungumzia chochote kuhusiana na ikia atashiriki kwenye mdahalo huo, na mnamo mwezi Machi Biden alisema ushiriki wake utategemea tabia za Trump.

"Nitafurahi kupambana naye," alisema Biden. "Ninajiandaa. Sijui ni lini," aliongeza.

Trump ambaye alikwishasema yuko tayari kupambana na Biden hata hivyo ametilia mashaka utayari huo wa mpinzani wake, ingawa siku ya Ijumaa alisisitiza tena kwamba yuko tayari kwa mdahalo huo... mahali popote, wakati wowote.

New York Trump awasili mahakani
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa katika mahakama ya uhalifu ya Manhattan kujibu moja ya kesi zinazomkabiliPicha: Jabin Botsford/REUTERS

Rais huyo wa zamani wa Marekani ambaye anamshutumu Biden kwa kutumia mfumo wa haki kuhujumu jitihada yake ya kurejea Ikulu ya White House, alipendekeza kufanyika kwa mjadala huo ama kwenye mikutano yake ya kampeni katika jimbo la Michigan wiki ijayo -- au hata siku ya jana ya Ijumaa.

Kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth, Trump alilalama "Nimekwama kwenye moja ya kesi nyingi zilizoko mahakamani dhidi yangu ambazo (Biden) alizianzisha ili kuingilia uchaguzi dhidi ya mpinzani wake wa kisiasa."

Biden na Trump walikutana kwenye midahalo miwili wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Soma pia; Biden, Trump wazoa ushindi kinyang´anyiro cha ´Jumanne Kuu´

Midahalo ya wagombea huwa ni hatua kubwa na ya muhimu katika mchakato wa uchaguzi nchini Marekani kwa miaka na mikaka, ambayo huwasaidia wapiga kura kuwatathmini wagombea.

Biden ambaye anamtaja Trump kama kitisho cha demokrasia aliwaambia waandishi wa habari mwezi uliopita kwamba makubaliano yoyote ya mdahalo na tajiri huyo wa majengo "yanategemea tabia yake."

Soma pia: Biden: Kampeni ya "Fanya Marekani Kuwa Kuu Tena" ni tishio kwa demokrasia